Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 04, 2022 Local time: 05:44

Israel yaongeza mashambulizi yake Gaza


Wapalestina wakipitia vifusi baada ya shambulizi lilisemekana kuwa la jeshi la Israel huko Rafah,Gaza Strip, July 11, 2014.

Mapigano yameongezeka wakati Israel inaendelea na siku ya nne ya mashambulizi yake Ijumaa huko Gaza, huku wapiganaji wa Palestina nao wakiendeleza mashambulizi ya roketi dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi. Kundi la Hamas limetoa onyo kwa mashirika ya ndege ya kimataifa kutotumia anga ya uwanja wa ndege wa Tel Aviv.

Kundi hilo ambalo lilisema linataka kuepuka madhara yoyote kwa abiria lilielekeza kombora moja kuelekea uwanja huo wa ndege Ijumaa. Hata hivyo, shughuli za uwanja huo wa ndege ziliendelea kama kawaida licha ya onyo hilo.

Mapigano yanayoendelea yamemfanya Rais Barack Obama wa Marekani kumpigia simu Alhamisi Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kueleza wasiwasi wake na kusema yuko tayari kusaidia katika majadiliano ya kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry alimpigia simu mwenzake wa Misri kuiomba nchi huyo kutumia ushawishi wake kuepusha kuendelea kwa uhasama huo. Misri ilikuwa sehemu kubwa ya majadiliano ya amani kati ya Israel na Hamas mwaka 2012.

XS
SM
MD
LG