Iran imesema itaendelea na juhudi za kutaka kuachiliwa huru kwa afisa wa zamani wa Iran aliyehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kushiriki katika mauaji ya wafungwa wa kisiasa nchini Iran.
“Uamuzi huu usio wa haki na wa kukasirisha haumalizi juhudi za kidiplomasia za Iran za kumrejesha na kumuachia huru raia huyu wa Iran, na tutatumia njia zote za kisheria na zilizopo”, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Nasser Kanaani alisema, bila ya kufafanua.
Jumanne iliyopita, mahakama ya rufaa ya Sweden iliidhinisha hukumu ya kukutwa na hatia pamoja na kifungo cha maisha kwa mauaji na uhalifu mkubwa dhidi ya sheria ya kimataifa kwa afisa wa zamani Hamid Noury.
“Tunapinga vikali hukumu hiyo na kile kilichotokea wakati wa kipindi kirefu cha raia huyu kizuizini, na haki zake za msingi hazijaheshimiwa katika magereza ya Sweden”, Kanaani aliuambia mkutano wa waandishi wa habari wa kila wiki. “Tunatumaini Sweden itachukua hatua kali kufidia makosa yake”.
Mapema mwezi Disemba, Iran ilianza kesi ya raia mmoja wa Sweden, Johan Floderus, aliyeajiriwa na Umoja wa Ulaya ambaye anashtakiwa kwa kuipeleleza Israel na “ufisadi duniani”, uhalifu ambao unapatiwa adhabu ya kifo.
Forum