Idadi ya waliofariki dunia kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa mashariki mwa Uganda imepanda hadi 17, msemaji wa serikali alisema Ijumaa, huku wengine zaidi ya 100 wamepotea.
Maporomoko hayo ya ardhi yalitokea siku ya Jumatano katika wilaya ya Bulambuli, kiasi cha kilomita 300 mashariki mwa mji mkuu Kampala, na darzeni ya nyumba kufukiwa katika vijiji kadhaa.
Picha za kwenye televisheni nchini humo zilionyesha maeneo makubwa yakiwa yamefunikwa na matope mazito ambako nyumba na shule zilikuwepo. Walionusurika walikuwa wakilia kwa kupoteza wapendwa wao huku waokoaji wakichimba kwenye tope kuwatafuta manusura.
Forum