Uamuzi huo unaonekana kuwa ushindi wa mapema kwa Iran, lakini pigo kwa Tehran kwa sababu Mahakama ya ICC haina mamlaka kuhusu mali za thamani yad ola bilioni 1.75 ambazo zilikamatwa kutoka kwenye benki kuu ya Iran.
Kaimu mshauri wa sheria Rich Visek, wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, amesema katika taarifa kwamba uamuzi huo umeshindwa kuzingatia sehemu kubwa ya kesi hiyo, hasa inapozingatia zaidi mali za benki kuu.
Wizara ya mambo ya nje ya Iran imeandika ujumbe wa Telegram kwamba imekubaliana na uamuzi huo, ikisema unaangazia uhalali wa msimaamo wake kuhusu tabia mbaya ya Marekani.
Uamuzi huo umetolewa wakati uhusiano kati ya Marekani na Iran ni mbaya baada ya kutokea mashambulizi ya kulipizana kati ya wanajeshi wanaoungwa mkono na Iran na wanajeshi wa Marekani nchini Syria, wiki iliyopita.
Uhusiano umekuwa mbaya baada ya jaribio la kufufua makubaliano ya program ya nyuklia, yam waka 2015 kati ya Iran na nchi nyingine zenye nguvu duniani kufeli, nah uku Iran ikiripoti kutoa ndege zake zisizo na rubani kwa Russia katika vita dhidi ya Ukraine.
Kesi hiyo ilianzishwa naTeheran dhidi ya Washington mwaka 2016 kwa madai ya kuvunja makubaliano ya urafiki yam waka 1955 kwa kuruhusu mahakama za Marekani kuzuia mali za kampuni za Iran. Pesa hizo zilikuwa azitumike kutoa fidia kwa waathirika wa ugaidi.
Jamhuri ya kiislamu ya Iran, imekuwa ikipinga shutuma kwamba inafadhili ugaidi kimataifa.