Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 02:25

HIV na Ukimwi inaweza kumalizika kama tishio la afya ya umma 2030; UNAIDS


Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS, Winnie Byanyima. Geneva, July 3, 2020.
Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS, Winnie Byanyima. Geneva, July 3, 2020.

Ugonjwa huo hatari umeua watu milioni 40.4 tangu kuanza kwa janga hilo mwaka 1981. “Takwimu katika ripoti hii zinaonyesha kuwa njia inayomaliza Ukimwi sio siri, lakini ni chaguo. Ni chaguo la kisiasa na kifedha,” alisema Winnie Byanyima, mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS

Virusi vya HIV na Ukimwi vinaweza kumalizika kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030 kama mataifa yanaweza kuwa na utashi wa kisiasa na msaada muhimu wa kifedha ili kuushinda kabisa, ripoti mpya iliyochapishwa Alhamisi inasema.

Ugonjwa huo hatari umeua watu milioni 40.4 tangu kuanza kwa janga hilo mwaka 1981. “Takwimu katika ripoti hii zinaonyesha kuwa njia inayomaliza Ukimwi sio siri, lakini ni chaguo. Ni chaguo la kisiasa na kifedha,” alisema Winnie Byanyima, mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS.

“Ripoti hiyo inaonyesha kuwa majibu ya HIV yanaweza kufanikiwa wakati yanatia nanga katika uongozi imara wa kisiasa,” alisema.

Ripoti hiyo iliyotolewa na Program ya Umoja wa Mataifa inayohusika na ukimwi (UNAIDS) inaonyesha mwaka 2022 watu milioni 39 duniani kote walikuwa wanaishi na virusi vya ukimwi ambapo milioni 1.3 waliambukizwa virusi hivyo na watu 630,000 walifariki kutokana na magonjwa yanayohusiana na Ukimwi.

Forum

XS
SM
MD
LG