Wapiganaji wa Hezbollah, ambao walikuwa wamefunika nyuso zao, waliruka mioto, kupiga risasi wakiwa wamepanda pikipiki, na kuhaaribu bendera za Israel zilizokuwa zimewekwa mlimani na ukuta uliowekwa kuigiza ukuta unaoitenganisha Lebanon na Israel.
Mazoezi hayo yamefanyika kabla ya siku ya ukombozi, inayofanyika kila mwaka, kuadhimisaha kuondoka kwa wanajeshi wa Israel kutoka kusini mwa Lebabon, May 25, 2000.
Mazoezi pia yamefanyika wakati mgogoro kati ya Israel na Palestina umeongezeka huko ukanda wa Gaza.
Kundi la wapiganaji la Hamas, ambalo linaidhibiti Gaza limekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na kundi la Hezbollah.
Jeshi la Israel limekataa kuzungumzia mazoezi hayo ya kundi la Hezbollah.