Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 02:00

Rais wa zamani wa Chad ahukumiwa kifungo cha maisha jela


Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre
Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:36 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mahakama nchini Senegal imemkuta na hatia rais wa zamani wa Chad Hissene Habre na shutuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu, uhalifu wa vita, na mateso, na imemhukumu kifungo cha maisha jela. Makundi ya kutetea haki yamepongeza hukumu hiyo ya kihistoria wakisema ni onyo kali kwa viongozi wanaotaka kuwanyanyasa raia wao.

Jaji mkuu Gberdao Gustave Kam wa Burkina Faso, alitangaza hukumu hiyo.

Mahakama ilimkuta na hatia Bw Habre kwa kuhusika moja kwa moja kuamuru watu kuwekwa kizuizini, kuuwawa, mateso na ukiukaji mwingine dhidi ya watu walotambuliwa kama wapinzani wa utawala wake.

Jaji Kam alisema Habre alisimamia miaka 8 ya ukandamizaji. Makundi ya kutetea haki yanasema Habre alihusika na mauwaji takriban elfu 40.

Wakati wa kutowa hukumu, jaji Kam alisema Habre alibuni na kuendeleza mfumo wa kutokhofia kushtakiwa na vitisho kama ndiyo mwenendo wa kisheria. Alikuwa mkuu wa utawala uliokuwa na mashaka mengi, kiasi kwamba yeye mwenyewe aliwageuka maafisa wake mwenyewe.

Mawakili wa waathiriwa kwenye kesi dhidi ya dikteta wa zamani Hissene Habre wa Chad
Mawakili wa waathiriwa kwenye kesi dhidi ya dikteta wa zamani Hissene Habre wa Chad

Waathirika wa utawala wa Habre na wanafamilia wa waathirika waliokuwepo mahakamani jana jumatatu walilia na kusheherekea baada ya Habre kuhukumiwa kifungo cha maisha.

Tumeshinda kwa uwezo wa mungu, alisema mwanamke mmoja, ambaye mumewe alikuwa mtumishi wa serikali ya Habre, na ambaye aliwahi kufungwa na kuteswa. Alifariki kabla ya kesi hio kuanza.

Mwanamke huyo anasema hana maneno ya kusemaa. Simba, mwanamume ambaye alijiona kama mungu hapa duniani, leo ameangushwa.

Habre hakusema lolote. Aliikunja mikono yake pamoja na kuwapungia wafuasi wake pale alipokuwa akiondolewa mahakamani.

Habre alikimbilia Senegal mwaka 1990 baada ya kuondolewa madarakani katika mapinduzi.

Kesi dhidi yake imechukuwa zaidi ya miaka 20 kuendeshwa. Mahakama maalum ya umoja wa Afrika ijulikanyo kama The Extraordinary African Chambers, iliundwa mwaka 2013 kulingana na mfumo wa kisheria wa Senegal na kufadhiliwa na jumuiya ya kimataifa.

Miongoni mwa wale walotowa ushahidi ni watu 69 walionusurika wakiwa kizuizini na kukumbwa na ukiukaji, ikiwa ni pamoja na mwanamke mmoje ambaye Habre alipatakana na hatia ya kumbaka mara nne.

Mawakili wa Habre wana siku 15 kukataa rufaa dhidi ya uamuzi huo.

XS
SM
MD
LG