Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Guinea Bissau imesema Umoja huo na washirika wake wa kimataifa wameridhishwa sana na jinsi uchaguzi wa rais wa nchi hiyo ulivyofanyika, wakati wafanyakazi wa uchaguzi wakihesabu kura katika taifa ambalo kawaida kutokea majaribio ya mapinduzi ya mara kwa mara.
Msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudumisha amani huko Guinea Bissau (UNIOBBIS) Vladmir Monteiro aliimabia Sauti ya Amerika kwamba watu waliojitokeza walikuwa wachache wakati wa asubuhi Jumapili, lakini maafisa wa uchaguzi waliweza kuwahimiza watu wengi kushiriki badaye siku hiyo.
Matokeo yanatarajiwa katika wiki moja. Wapiga kura wanatarajia rais mpya atawaletea uthabiti wa kiasi fulani nchini humo, ambayo inatumiwa kama kituo cha usafiri cha biashara haramu ya madawa ya kulevya kutoka Amerika ya Kusini pamoja na kwamba viongozi wa kiraia na kijeshi wa nchi siku zote wamekuwa wakipambana kutaka kuchukua madaraka.