Timu ya taifa ya Ghana hatimaye imepata nafasi ya kuingia raundi ya pili baada ya kuichapa Afrika Kusini mabao 2-1 na Simba wa Teranga Senegal wameaga michuano hiyo baada ya kujikuta wakiangukia pua mbele ya Algeria kwa kushindwa 2-0. Kwa hivyo kundi la kifo lililokuwa wazi hatimaye Ghana na Algeria wameweza kufanikiwa kuingia raundi ya pili ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika 2015 kutoka kundi C.