Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 02:39

Jumuia ya Kimataifa yalani uvamizi wa Israel dhidi ya meli za misaada


Jumuia ya kimataifa imelaani uvamizi wa Israel dhidi ya meli zilizokuwa zinasafirisha msaada hadi ukanda wa Gaza.

Viongozi na maafisa wa nchi za kiarabu ni miongoni walioongoza katika kujibu kwa hasira uvamizi wa Israel dhidi ya mlolongo wa meli zilizkua zinasafirisha msaada wa dharura kutoka Ulaya hadi kwa wananchi wa Gaza.

Umoja wa nchi za Kiarabu umeitisha mkutano wa dharura kujadili mzozo huo hapo kesho ili kujibu maombi ya baadhi ya wanachama wake kutaka kutolewa kwa taarifa ya pamoja kulani kitendo hicho cha Israel.

Katibu mkuu wa umoja wa nchi za kiarabu Amr Moussa ametoa wito wa kutathminiwa upya uhusiano na Israel
“Nchi za kiarabu zinaendelea kuhisi kitisho cha ugomvi kati ya nchi za kiarabu na Israel, ukaliaji wa ardhi za waarabu unaofanywa na Israel, na Israel kuzuia kuundwa kwa taifa litakaloweza kiujitegemea la wa-Palestina.

Mfalme wa Qatar Sheikh Hamad bin Jassim amelaani vikali uvamizi huo wa Israel dhidi ya meli za misaada akiomba tukio hilo litumiwe kama kichoche cha kuondoa vizuizi vya Israel na misri dhidi ya ukanda wa gaza.
“Uhalifu umetendeka dhidi ya walofika kueleza uungaji mkono wao na wananchi wa Gaza na hii inakumnbusha kwamba kuna vizuizi visivyo vya haki vinavyosababisha machungu makubwa kwa wananchi wa Gaza”.

Wakati huo huo waziri mkuu wa Lebanon Saad Hariri ambae nchi yake ni mwenyekiti wa mwezi huu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa amemuomba mjumbe wake kuitisha mkutano wa dharura wa baraza hilo kujadili hali hiyo.
Baada ya mkutano mjini Damuscus bw Hariri na rais Basher al Assad wa Syria kwa pamoja wamelaani uvamizi wa Israel dhidi ya meli hizo na kueleza kua ni uhalifu wa kikatili na kuuhimiza Umoja wa Mataifa kukomesha kile wanachosema ni ukiukaji mkubwa wa Israel wa haki za binadam. Mjini Khartoum rais Omar al Bashir aliambia kituo cha televisheni cha Al Jazeera kwamba ni lazima kwa mataifa ya kiarabu kukata kabisa uhusiano wote na Israel.

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ameeleza kitendo hicho kua ni “ugaidi wa Kitaifa”, na Uturuki imemrudisha balozi wake huko Israel.

Rais wa Marekani Barack Obama amemuhimiza waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutafuta ukweli wote juu ya jinsi kitendo hicho kilichosababisha vifu vya wanaharakati 9. White House imeelza kwamba Bw Obama ameeleza masikitiko yake kutokana na walofariki katika shambulio hilo na ni muhimu kufahamu jinsi mambo yalivyotokea.
Kwa upande wake kamishna mkuu wa haki za binadamwa Umoja wa Mataifa Navi Pillay aliungana na jumuia ya kimataifa kulaani uvamizi huo

XS
SM
MD
LG