Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 22:25

Rais wa Gabon akataa kuhesabiwa tena kwa kura


Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba

Rais wa Gabon, Ali Bongo, anayeshutumiwa na upinzani kwa wizi wa kura, siku ya Jumatano alipinga wito wa kuhesabiwa tena kwa kura za uchaguzi wa rais na kusema kwamba hana mamlaka ya kutoa amri hiyo.

Wafuatiliaji wa Umoja wa Ulaya huko Gabon wamesema kulikuwa na hali isiyo ya kawaida katika matokeo ya kura hiyo, iliyomuonyesha Bongo akimshinda mpinzani wake Jean Ping, Kwa kura chache.

Ujumbe huo wa Umoja wa Ulaya umesema una tashwishi kuhusu matokeo ya uchaguzi huo kwenye jimbo Upper Ogooue, ambalo ni ngome ya rais Bongo, aliyeshinda asili mia 95 ya kura, kukiwepo asili mia 99 ya wapiga kura wakijitokeza. Upinzani umesema idadi ya kura zilizohesabiwa katika jimbo hilo liliongezwa kwa kiwango kikubwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG