Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 14:43

FAO inatoa wito wa kuongeza uzalishaji chakula duniani


Mkulima wa Afrika kusini
Mkulima wa Afrika kusini

“Kuungana dhidi ya Njaa” ndio kauli mbiu iliyochaguliwa mwaka huu kuadhimisha siku ya chakula duniani na shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa mataifa, FAO . Wawakilishi wa nchi wanachama wa FAO walishiriki katika sherhe za kuadhimisha siku hii kwenye makao makuu ya shirika mjini Roma.

Akiwahutubia wajumbe, mkurugenzi wa FAO Jacques Diouf alisema kauli mbiu ya mwaka huu inaonyesha kwamba usalama wa chakula si jukumu la upande mmoja bali la wote.

Alisema njaa inaenedelea kua tatizo kubwa sana licha ya kuwepo na chakula kingiu duniani matumaini mazuri ya uchumi na bei za chini kabisa za chakula.

“Hali ya kipekee iliyopo sasa imetokea kwasababu badala ya kupambana na sababu za kimfumo za kutokuwa na usalama wa chakula, dunia imedharau sera za maendeleo ya kilimo, sera zinazopelekea uwekezaji mdogo hasa katika sekta hiyo katika nchi zinazoendelea”,alisema bw Diouf.

Diouf amesema watu milioni 925 wanaishi katika hali sugu ya njaa na utapia mlo. Idadi hiyo alisema inawakilisha kupunguka kwa kiasi Fulani kulingana na mwaka 2009, lakini bado haikubaliki kua juu namna hiyo.

Mkurugenzi wa FAOaliongeza kusema kwamba nchi 100 zinahitaji msaada wa dharura kujenga upya uwezo wa kilimo cha uzalishaji na mataifa 30 yanakabiliwa na mzozo wa chakula.

XS
SM
MD
LG