Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 03:28

Rais wa Uturuki aamuru ndege za kijeshi kulinda doria


Turkish President Recep Tayyip Erdogan right, wipes his tears during the funeral of Mustafa Cambaz, Erol and Abdullah Olcak, killed Friday while protesting the attempted coup against Turkey's government, in Istanbul, July 17, 2016.
Turkish President Recep Tayyip Erdogan right, wipes his tears during the funeral of Mustafa Cambaz, Erol and Abdullah Olcak, killed Friday while protesting the attempted coup against Turkey's government, in Istanbul, July 17, 2016.

Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan, siku ya Jumatatu aliamuru ndege za kijeshi za nchi hiyo aina ya F-16 zilinde doria katika anga ya nchi hiyo usiku kucha, hata ingawa hakukuonekana ishara zozote mpya za mapambano yoyote na serikali, baada ya jaribio la kuipindua serikali hiyo siku ya Ijumaa. Pamoja na hayo, serikali ya Ankara Jumatatu ilisitisha mpumziko ya wafanyakazi milioni tatu wa serikali na kuwataka warudi kazini mara moja.

Wakati huo huo, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, alisema Jumatatu kuwa anaunga mkono kufunguliwa mashtaka kwa watuhumiwa wa jaribio la kuipindua serikali ya Uturuki, lakini akaonya dhidi ya kutumia mbinu zinazokiuka sheria katika juhudi za kuleta hali ya utulivu nchini humo. Kerry amewaambia waandishi wa habari baada ya kukutana na mawaziri wenzake kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels kuwa Marekani inasimama imara na upande ambao umechaguliwa na wananchi wa Uturuki.

Aidha alisema kuwa ni muhimu kuhakikisha kuwa kuna utulivu na amani nchini kote. Aliitaka serikali ya uturuki kuheshimu taasisi za kikatiba na sheria za nchi.Shirika la habari linalomilikiwa na serikali, ANADOLU, liliripoti kuwa maafisa 8,777 wamesimamishwa kazi na wafanyakazi 6,000 wa mahakama na jeshi, wametiwa kizuizini kufuatia jaribio la kuipindua serikali siku Ya Ijumaa, hatua ambayo imelaaniwa na baadhi ya viongozi wa kimataifa ambao wameonya kwamba huenda ikawa na athjari kikatiba.

XS
SM
MD
LG