Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 02:13

Colombia yatangaza hali ya dharura kutokana na moto uliounguza darzeni ya misitu


Wafanyakazi wa zimamoto wakipambana na moto wa msituni katika mlima huko Bogota, Colombia, Januari 24, 2024. REUTERS/Antonio Cascio
Wafanyakazi wa zimamoto wakipambana na moto wa msituni katika mlima huko Bogota, Colombia, Januari 24, 2024. REUTERS/Antonio Cascio

Colombia imetangaza hali ya dharura katika mikoa miwili wakati darzeni ya misitu imeungua  katika  eneo kubwa  la nchi hiyo na kuuacha mji mkuu ukigubikwa na moshi huku joto likiwa juu zaidi likihusishwa na matokeo ya hali ya hewa ya El Nino.

Colombia imezima mioto zaidi ya mia moja mwezi huu, lakini 25 inaendelea kuwaka, kulingana na takwimu kutoka kitengo cha Usimamizi wa Hatari za Maafa ya Kitaifa (UNGRD) siku ya Jumatano.

Katika idara za Santander na Cundinamarca, ambako, mji mkuu, Bogota, upo, mioto hiyo imeteketeza kiasi cha hekta 600 za misitu na hali ya dharura imetangazwa.

Hatua hizo za dharura zimeruhusu fedha kutolewa ili “kwa haraka kukabiliana na athari hasi za rasilimali za asili zinazomilikiwa na Idara hiyo,” alisema Gavana wa Cundinamarca Jorge Emilio Rey.

Zaidi ya nusu ya manispaa mbalimbali za nchi hiyo ziko kwenye tahadhari ya juu sana kutokana na tishio la moto, huku maeneo yanayozunguka mji mkuu yakiwa yameathirika zaidi.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG