Mshindi huyo wa Kombe la Dunia wa Argentina alihamia Stamford Bridge kwa ada iliyoweka rekodi ya Uingereza yenye thamani ya pauni milioni 107 katika siku ya mwisho.
Pande zote mbili zilikuwa zimekwama katika mazungumzo tangu Kombe la Dunia, huku Chelsea wakimfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuwa mlengwa wao mkuu baada ya kufurahishwa na uchezaji wake nchini Qatar.
Mazungumzo kuhusu hatua hiyo ambayo yaliendelea kwa muda mrefu wa Januari na Jarida moja la Ureno sasa limefichua mvutano mkubwa kati ya kambi hizo mbili zilipokutana kuzungumza kuhusu Fernandez na jinsi Benfica walivyoshinikiza kwa Mateo Kovacic kujumuishwa katika mpango wa kubadilishana.
Hata hivyo The Blues -Chelsea inakanusha taarifa hizo kutoka Ureno.
Facebook Forum