Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 17:12

Bunge la Uingereza launga mkono mswada wa kuhalalisha usaidizi wa kifo


Kim Leadbeater, Mbunge wa Spen Valley, akitembea siku ya maandamano ya kuunga mkono mswada wa usaidizi kufa, mjini London, Uingereza, Novemba 29, 2024. REUTERS/Mina
Kim Leadbeater, Mbunge wa Spen Valley, akitembea siku ya maandamano ya kuunga mkono mswada wa usaidizi kufa, mjini London, Uingereza, Novemba 29, 2024. REUTERS/Mina

Bunge la Uingereza limepiga kura kuukubali mswada wa kuhalalisha usaidizi wa kifo siku ya Ijumaa, na kufungua nafasi kwa mjadala zaidi wa miezi kadhaa kuhusiana na suala ambalo limeigawa nchi na kuzua maswali kuhusiana na kiwango cha uuguzi na uponyaji.

Baada ya mjadala mkali katika baraza la chini la bunge, wabunge 330 walipiga kura kuunga mkono mswada wa “wagonjwa mahututi watu wazima (wanaokaribia kufa) na wabunge 275 wakipinga.

Chini ya mswada huo watu wenye matatizo ya akili, wagonjwa watu wazima wanaokaribia kifo nchini Uingereza na Wales ambao wametathiminiwa na madaktari kuwa na hadi miezi sita ya kuishi waweze kupewa haki ya kuchagua kumaliza maisha yao kwa msaada ya kitabibu.

Wale wanaounga mkono mswada huo wamesema inahusiana na ufupishaji kifo kwa wale ambao ni wagonjwa mahututi na kuwapa udhibiti zaidi.

Lakini wapinzani wamesema wagonjwa wenye hali tete wanaweza kuhisi haja ya kumaliza maisha yao kwa hofu ya kuwa mzigo kwa familia zao na jamii, badala ya uzima wao.

Wengine wameelezea wasiwasi kwama hakukuwa na muda wa kutosha wa kutathimini mswaada huo kabla ya kupiga kura.

Forum

XS
SM
MD
LG