Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 31, 2023 Local time: 19:42

Boko Haram yasema itaendelea na mashambulizi Nigeria


mmoja wa walionusurika na shambulizi la bomu linalosadikiwa kufanywa na boko horam akiwa hospitali

kundi hilo limedai kuendelea na mashambulizi yake katika maeneo mbalimbali nchini Nigeria.

Kiongozi wa kundi la kiislamu lenye msimamo mkali la Boko Haram ameitolea changamoto adhma ya rais Jonathan wa Nigeria ya kuvunja kundi hilo katika ujumbe kwa njia ya sauti ulirekodiwa kwenye internet.

Ujumbe huo umetolewa katika mtandao wa you tube umeonesha picha ya imamu Abubakar Shekau akiwa na bunduki aina ya Kalashnivok.

Katika ujumbe wake amesema rais Goodluck Jonathan atajifunza kuwa hawezi kulishinda kundi la boko haram na akaonya kwamba wanamgambo watafanya shambulizi tena.

Shekau amesema boko haram ilifanya mashambulizi mfululizo katika mji wa kaskazini wa Kano januari 20 na kuuwa watu 185.

Kundi hilo limekuwa limetaaabisha Raia wa Nigeria kwa miezi kadhaa sasa

XS
SM
MD
LG