Wanadiplomasia wanasema baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linakutana leo kujadili majaribio ya karibuni ya makombra ya Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini imesha fyatua makombora matatu katika bahari ya Japan Jumatatu kutoka katika jimbo la Hwanghae, lililopo katika mwambao wa mashariki wa nchi hiyo.
Mkuu wa majeshi ya muungano ya Korea Kusini ameyataja makombora hayo kama makombora ya Rodong, yenye uwezo wa kusafiri umbali wa kilometa 1,000.
Wizara ya ulinzi ya Japan inasema makombora hayo yalidondoka katika ukanda wa mahsusi wa kiuchumi katika eneo hilo ambalo linajulikana kama bahari ya mashariki.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema majaribio ya makomboroa ya Korea kaskazini yamekuwa ya kawaida sana katika miezi kadhaa iliyopita.