Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:11

Baba Mtakatifu kuwasili Kenya, Jumatano


Mabango ya ujio wa Baba Mtakatifu Francis mjini Bamako, Mali.
Mabango ya ujio wa Baba Mtakatifu Francis mjini Bamako, Mali.

Kiongozi wa kanisa katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Francis, anatarajiwa kuanza ziara ya kihistoria ya siku tatu nchini Kenya kabla ya kwenda nchi za Uganda na Afrika ya kati. Kulingana na polisi na maskofu wa kanisa katoliki mjini Nairobi mipango yote imekamilika ya kumkaribisha Baba Mtakatifu Francis ikiwa ni pamoja na kuimarishwa kwa hali ya usalama kote mjini Nairobi.

Taarifa zaidi zilisema Baba Mtakatifu Francis anatarajiwa kuwasili Nairobi saa 5.00 jioni siku ya Jumatano kabla ya kumtembelea mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi. Barabara zote muhimu mjini Nairobi zimefungwa na zaidi ya mafisa 10,000 wa polisi wamewasili Nairobi kuhakikisha kuna asalama wa kutosha wakati wa ziara ya siku tatu ya kiongozi huyo wa kanisa katoliki. Inspekta mkuu wa polisi Bwana Boinet alisema hakuna magari yatakayo-ruhusiwa kuingia katikati ya mji mkuu kama hatua mojawapo ya usalama

Katika muda wa siku kadha zilizopita maelfu kwa maelfu ya waumini wa kanisa katoliki wamekuwa wakijianda kumpokea Baba Mtakatifu.Wengi wao wamemiminika mjini Nairobi kushuhudia sherehe hizo.

Kulingana na ratiba rasmi iliyotolewa na serikali na maaskofu wa kanisa katoliki, Baba Mtakatifu Francis atakuwa na shughuli nyingi mjini Nairobi. Ataongoza misa katika sehemu tatu tofauti, kuhutubia vijana na kutembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira-UNEP.

Pope Francis
Pope Francis

Kwa mujibu wa maskofu wa kanisa katoliki nchini Kenya, Baba Mtakatifu vile vile anatarajiwa kuzungumzia maswala yanayohusiana na utawala bora, ujirani mwema, rushwa, ukabila, haki za binadamu na magonjwa ya HIV na ukimwi lakini baadhi ya waumini la kanisa katoliki wanamtarajia kuzungumza kuhusu matumizi ya mipira ya kondom.

Hata hivyo Maskofu wa kikatoliki wanapinga uwezekano wa Baba Mtakatifu kukutana na mapadri waliooa au maseja kabla ya kuondoka Nairobi siku ya Ijumaa kuelekea nchini Uganda. Baba Francis atatembelea na kuongoza misa katika mtaa wa watu masikini wa Kangemi, viungani vya mji mkuu wa Nairobi. Kanisa kwenye eneo hilo limefanyiwa ukarabati na kuwekwa taa mpya. Pia serikali siku ya Jumanne imetangaza kuwa siku ya Alhamisi itakuwa ni siku ya mapumziko kote nchini.

XS
SM
MD
LG