Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 11:24

Viongozi wa Afrika wahudhuria kikao cha AU


Viongozi wa mataifa ya Afrika katika mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia, mwaka jana.
Viongozi wa mataifa ya Afrika katika mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia, mwaka jana.

Viongozi kadhaa wa Afrika wako Addis Ababa leo Jumamosi kwa ajili ya ufunguzi wa kikao cha Umoja wa Afrika.

Rais wa Zimbabwe na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Robert Mugabe amefungua kikao hicho ambacho mwaka huu kinalenga masuala ya haki za binadamu barani humo.

Mzozo wa Burundi uko juu katika ajenda ya viongozi. Umoja wa Afrika unafikiria mpango wa kupeleka kikosi cha walinzi wa amani 5,000 nchini humo ili kudhibiti ghasia ambazo zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 400. Serikali ya Burundi inasema itawazuia wanajeshi wowote wa kigeni ambao watajaribu kupelekwa katika taifa hilo la Afrika ya Kati.

Mzozo wa Burundi ulianza April mwaka jana pale rais Pierre Nkurunziza aliposema kuwa atawania uongozi kwa muhula wa tatu. Makundi ya haki za binadamu yameshutumu ukamataji unaofanywa na serikali kwa waandishi wa habari na waandamaji ikiwa ni juhudi za kukandamiza upinzani wa kisiasa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon ambaye anahudhuria kikao hicho, ameonya kwamba “viongozi ambao wanakaa tu wakati raia wanauawa kwa jina lao ni lazima wawajibishwe. Amesema mzozo nchini Burundi unahitaji suluhisho la haraka.

Miongoni mwa viongozi wa Afrika wanaohudhuria kikao cha ufunguzi kinachofanyika katika mji mkuu wa Ethiopia ni rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma na rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sissi.

XS
SM
MD
LG