Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 05:42

Al Shabaab yashambulia kambi ya wanajeshi wa AU katika mkoa wa Shabelle


Askari wa Umoja wa Afrika wakati wa mapambano na Alshabab huko Mogadishu.
Askari wa Umoja wa Afrika wakati wa mapambano na Alshabab huko Mogadishu.

Kundi la al Shabaab la Somalia lilishambulia kambi ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika katika mkoa wa Shabelle katikati mwa nchi hiyo, mzee wa eneo hilo na kundi hilo lilisema siku ya Jumanne, na mkazi mwingine alisema raia watatu walikufa katika mapigano hayo.

Mkazi mmoja anayeishi katika kijiji kilicho karibu na eneo la tukio, alisema baadaye aliona helikopta mbili zikipita na milio ya risasi ikitoka kwao.

"Tuliamshwa na milipuko mikubwa mapema asubuhi. Milipuko hiyo ilikuwa katika kituo cha Umoja wa Afrika. Milio ya risasi ilifuata," mzee wa eneo hilo Mohamed Nur aliiambia Reuters kwa simu kutoka El Baraf, kiasi cha kilomita 130 hadi kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu.

Al Shabaab, ambayo imekuwa ikipigana kwa miaka mingi kuiangusha serikali kuu na kusimika utawala wake kwa kuzingatia tafsiri yake kali ya sharia ya Kiislamu, ilidai kuhusika na shambulio hilo.

XS
SM
MD
LG