Wanachama wa kundi moja la usalama Nigeria wamefanikiwa kukamata na kutegua bomu linaloaminika lilikuwa la kujitoa muhanga ambapo mwanamke mmoja alikuwa anaeelekea sokoni katika mji wa Maiduguri jimboni Borno.
Maafisa wa kundi linalofuatilia masuala ya usalama wamewaambia wanahabari kwamba walimsimamisha binti mmoja katika kizuizi cha barabarani ambaye alikuwa ameficha mlipuko kwenye hijabu aliyokuwa amevalia.
Kundi la Boko Haram limekuwa likiwatumia wanawake zaidi na zaidi katika mashambulizi ya kujitoa muhanga.
Jumatatu mashahidi mjini Maiduguri wamesema milipuko miwili ililipuka kwenye soko lenye mkusanyiko wa watu ambapo wanawake wawili walijitoa muhanga na kuua darzen ya watu wiki moja iliyopita.
Katika shambulio la Jumatatu mashahidi wanasema watu watano walikufa.