Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:38

Afrika Kusini, Nigeria nje ya Kombe la Dunia


Mchezaji wa Ufaransa Yoann Gourcuff, akituliza mpira kifuani mbele ya Steven Pienaarna na Katlego Mphela,wa Afrika Kusini katika mechi yao Jumanne ambapo Afrika Kusini ilishinda 2-1 huko Bloemfontein,(AP Photo/Hassan Ammar)
Mchezaji wa Ufaransa Yoann Gourcuff, akituliza mpira kifuani mbele ya Steven Pienaarna na Katlego Mphela,wa Afrika Kusini katika mechi yao Jumanne ambapo Afrika Kusini ilishinda 2-1 huko Bloemfontein,(AP Photo/Hassan Ammar)

Afrika Kusini imekuwa nchi ya kwanza mwenyeji wa kombe la dunia kuaga mashindano

Afrika Kusini imekuwa nchi ya kwanza mwenyeji wa kombe la dunia kuaga mashindano hayo licha ya kuwafunga Ufaransa bao 2-1.

Mabao ya Afrika Kusini yalifungwa na Bongani Khumalo na Katlego Mphela na bao la kufutia machozi la Ufaransa lilifungwa na Florent Malouda kunako dakika ya 70.

Nao wawalkilishi wengine wa Afrika Nigeria wameaga mashindanoi hayo baada ya kutoka sare 2-2 na Korea Kusini.

Matokeo hayo yameipa Korea Kusini nafasi ya kusonga mbele kwa mara ya kwanza nje ya ardhi yao kwenye kombe la dunia.

Katika mechi nyingine ya kundi A Jumanne Uruguay iliifunga Mexico bao 1-0 huko Rustenburg na matokeo hayo yamezipeleka timu hizo zote mbili kwenye raundi ya pili.

Luis Suarez alifunga bao pekee na la ushindi kwa Uruguay kunako dakika ya 43 baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya Edinson Cavani.

Uruguay wamemaliza wakiongoza kundi hilo wakiwa na pointi saba wakati Mexico na Afrika Kusini wamemaliza na pointi nne kila mmoja na Ufaransa iliyocheza fainali miaka minne iliyopita imeshika mkia na pointi moja.

Mexico imefanikiwa kusonga mbele kewa tofauti ya magoli Afrika Kusini imeruhusu mabao 5 ya kufungwa wakati Mexico imefungwa mabao 2 tu.

Alikuwa ni mchezaji Obafemi Martins anayechezea Wolfsburg ya Ujerumani aliyeingia katika kipindi cha pili ambae alikosa nafasi kadhaa za wazi.

Pambano hilo ambalo Nigeria alikuwa akihitaji ushindi wa mabao 3 ili isonge mbele ilijikuta ikikosa nafasi kadhaa za wazi hasa katika kipindi cha pili lakini walishindwa kuingiza mpira wavuni.

XS
SM
MD
LG