Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 07:32

Mpinzani wa al-Bashir ajitoa katika uchaguzi ujao


Mpinzani wa al-Bashir ajitoa katika uchaguzi ujao
<!-- IMAGE -->

Maafisa huko Sudan kusini wanasema Yasir Arman, mgombea mkuu wa urais na mpinzani wa al-Bashir, katika uchaguzi ujao amejitoa kwenye kinyang’anyiro hicho. Maafisa kutoka kundi la zamani la uasi la Sudan People’s Liberation Movement-SPLM, wanasema mgombea wao Yasir Arman, amejitoa katika uchaguzi huo.

Shirika la habari la Reuters, linamkariri makamu mwenyekiti wa chama hicho, Rick Machar, akisema hatua hiyo ni muhimu kwa sababu ya utata wa uchaguzi na kuendelea kwa mzozo huko Darfur. Arman alionekana mtu mwenye uwezo wa kupambana na Rais wa sasa Omar al-Bashir, katika kura ya kitaifa ambayo inaanza April 11.

Katika taarifa ya pamoja ya Jumatano, Marekani, Uingereza na Norway walieleza wasiwasi wao kuhusu masharti ya uhuru wa kisiasa kufuatia uchaguzi wa Sudan, na walitaka upigaji kura ufanyike kwa haki na amani.

Siku ya Jumanne, kundi la International Crisis Group, lilikishutumu chama tawaka nchini Sudan cha National Congress Party-NCP, kwa kujaribu kuvuruga uchaguzi.

XS
SM
MD
LG