Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 07:40

Baadhi ya maeneo Burundi yakumbwa na njaa


Njaa iliyoikumba mkoa wa Kirundo nchini Burundi inadaiwa ni kiangazi pamoja na matumizi mabaya mazingira hasa ukataji miti.

Haya yalisemwa na msemaji wa jeshi la Polisi nchini Burundi Channel Nravaganya, alipokuwa akizungumza na Sauti ya Amerika.

Alielezea kuwa baada ya kufanya ziara katika eneo hilo maafisa wa idara za usalama huko Burundi wamewashauri wananchi wapande miti na kuomba wahisani wawasaidie.

Mamia ya wakazi wa mkoa huo wameripotiwa kukimbilia nchi jirani ya Rwanda na amesema kuwa wamepeleka majeshi katika eneo hilo kwasababu hivi sasa Burundi ni nchi ya amani na majeshi yanaweza kusaidia kwenye majanga ya kitaifa.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG