Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 25, 2023 Local time: 16:48

Utawala wa kijeshi wa Niger watangaza baraza la mawaziri.


Utawala wa kijeshi wa Niger umetangaza baraza la muda la mawaziri 20 kutumika mpaka uchaguzi ufanyike.

Utawala huo umesema katika taarifa yake watano kati ya mawaziri hao wapya ni wanajeshi. Shirika la habari la Ufaransa linasema kuwa wanawake watano pia waliteuliwa kushika wadhifa katika baraza hilo.

Kiongozi wa utawala huo Meja Salou Djibo alisema Jumapili kuwa hakuna kiongozi yeyote wa utawala huo atakayeruhusiwa kugombea katika uchaguzi wa rais.

XS
SM
MD
LG