Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 14:23

Viongozi wa AU waizungumzia mzozo wa Darfur


Jopo la Umoja wa Afrika lililopewa jukumu la kupendekeza namna ya kutanzua mzozo wa miaka sita wa mkoa wa Darfur magharibi mwa Sudan linasema mahakama maalum ya kusikiliza kesi za wanaotuhumiwa na uhalifu na mateso huko Darfur ni jambo la kupewa umuhimu mkubwa zaidi.

Jopo hilo la maafisa wa vyeo vya juu linaongozwa na rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki liliwasilisha ripoti yake mbele ya mkutano wa viongozi wa afrika mjini Abuja.

Akihutubia mkutano huo wa Abuja ulioongozwa na rais Umaru Yar’Adua wa Nigeria, rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki alisema kuna njia moja pekee ili utaratibu uweze kua wa kuaminika na kukubaliwa na wananchi wa Darfur.

Mbeki alisema , “Jopo linapendekeza makubaliano ya pande zote za Sudan, umoja wa Afrika unalazimika kuteua mahakimu na wachunguzi kutoka nje ya Sudan ambao watawasaidia wenzao wa Sudan kufanya uchunguzi, kuhukumu na kutanzua vita na uhalifu ulotendwa wakati wa vita vya Darfur.”

Umoja wa Mataifa unasema takriban watu laki tatu wameuwawa na milioni mbili na laki saba kutoroshwa makwao tangu waasi wa makabila ya wachache huko Darfur kutangaza uwasi dhidi ya serekali ya Khartoum inayoongozwa na waarabu hapo Febuari 2003.

XS
SM
MD
LG