Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 19:23

Obama Asaini Mswada wa Kuinua Uchumi


Chini ya mwezi mmoja baada ya kuingia madarakani, Rais Barack Obama alifunga safari Jumanne hadi Denver Colorado, ambapo alisaini mswada wa dola bilioni 787 utakaosaidia ufufua uchumi wa Marekani.

Bwana Obama amesema hicho ni kiasi kikubwa cha fedha za kuufufua uchumi katika historia ya taifa hili. White House inasema mpango huo utasaidia kubuni au kuokoa nafasi za kazi milioni tatu na nusu, kupunguza kodi kwa asilimia 95 ya wamarekani, na kuwekeza katika elimu, nishati, afya na miundombinu.

Hata hivyo, Bwana Obama ameonya kuwa hatua hiyo haimaanishi kuwa huu ndio mwisho wa matatizo ya uchumi Marekani. Ameonya pia kuwa huenda kukawa na vizingiti kadhaa katika kufanikisha hilo, na kwamba ni safari itakayohitaji nidhamu na uwajibikaji kwa pande zote mbili, serikali na sekta binafsi.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG