Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 16, 2025 Local time: 19:52

Rais Trump ameitishia Umoja wa Ulaya kwa ushuru wa asilimia 200 kwenye mvinyo


Rais Trump amekuwa akipigana vita vya ushuru wa biashara na washirika wake ikiwemo Canada na EU.
Rais Trump amekuwa akipigana vita vya ushuru wa biashara na washirika wake ikiwemo Canada na EU.

Rais wa Marekani Donald Trump leo Alhamisi aliitishia Umoja wa Ulaya kwa ushuru wa asilimia 200 kwenye mvinyo, Champagne na aina nyingine ya pombe zinazotengenezwa katika nchi 27 wanachama wa umoja huo, baada ya EU kuweka ushuru wa asilimia 50 kwa Whiskey ya Marekani.

Trump aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kwamba EU ni moja ya mamlaka ya kodi ya chuki na yenye unyanyasaji na ushuru duniani. Alisema iliundwa mwaka 1993 kwa lengo pekee la kutumia fursa ya Marekani kiuchumi.

Katika mwezi uliopita, Trump amekuwa akipigana vita vya ushuru wa hapo kwa hapo, na washirika wake wakubwa wa biashara - Mexico, Canada, China na EU katika kile anachosema ni juhudi za kuzuia mtiririko wa dawa za kulevya, hasa Fentanyl, ndani ya Marekani kutoka Mexico na Canada, na pia kuwashawishi wazalishaji kufunga kazi zao nje ya nchi na kuzihamishia Marekani ili kubuni ajira nyingi Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG