Togo kesho Jumatatu inafanya uchaguzi wa bunge baada ya mageuzi ya katiba yenye mgawanyiko mkubwa ambayo wapinzani wanasema yanafungua njia kwa Rais Faure Gnassingbe kuongeza zaidi utawala wa miongo kadhaa wa familia yake.
Katika uongozi wa taifa hilo dogo la Afrika Magharibi kwa karibu miaka 20, Faure Gnassingbe alimrithi baba yake Gnassingbe Eyadema, ambaye alitawala kwa karibu miongo minne.
Wakosoaji wanasema kuwa nasaba ya kisiasa katika taifa hilo dogo la Afrika Magharibi itaongezeka kutokana na mageuzi hayo. Watu katika mitaa ya pembeni mwa mji mkuu Lome waligawanyika juu ya uchaguzi, jukumu la kiongozi wa Togo, na nani anapaswa kuongoza.
Raia mmoja anayepaka rangi majengo Komlan Gato alisema ana matumaini kuwa kura hiyo inaweza kumleta kiongozi mpya lakini hakuwa na uhakika kuhusu uwepo wa haki katika sanduku la kura.
Forum