Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 11:08

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan ametangaza kufanya maandamano ya amani dhidi ya serikali


Waziri Mkuu wa zamani wa pakistan, Imran Khan
Waziri Mkuu wa zamani wa pakistan, Imran Khan

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan alitangaza Jumapili kwamba ataongoza maandamano ya amani dhidi ya serikali kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Islamabad baadae wiki hii kushinikiza madai yake ya uchaguzi mpya.

Khan aliwaomba wafuasi wa chama chake cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) na wa-Pakistan kwa ujumla kufika mjini ili kujiunga na mkutano wake unaoanza Jumatano akisema hatimaye utageuka kuwa maandamano ya kkupinga na kuendelea kushinikiza hadi matakwa yake yatakapotekelezwa.

Muungano unaoongozwa na upinzani ulimuondoa madarakani mchezaji huyo wa zamani wa Kriketi aliyegeuka kuwa mwanasiasa aliondolewa madarakani mwezi uliopita katika kura ya bunge ya kutokuwa na Imani nae na hivyo kuhitimisha serikali yake iliyodumu kwa takribani miaka mine. Mpinzani mkubwa wa Khan wa kisiasa, Shehbaz Sharif, alichukua nafasi yake kama mkuu wa muungano mpya unaotawala.

“hatutaikubali kamwe katika hali yoyote serikali hii, Khan aliuambia mkutano wa wanahabari kwa njia ya televisheni katika mji wa kaskazini-magharibi wa Peshawar wakati akitangaza mpango wake wa maandamano hayo. Aliionya mamlaka dhidi ya kuzuia kwa nguvu maandamano hayo. Kubaki Islamabad tutabaki huko hadi watakapovunja mabunge hayo na kutangaza tarehe ya uchaguzi wa wazi ambao hautaingiliwa na mataifa ya kigeni”.

Waziri wa habari Marriyum Aurangzeb alikosoa wito wa Khan wa maandamano na kukataa ombi lake la uchaguzi wa mapema akisema hawezi kudhulumu serikali kutangaza uchaguzi mkuu kwa wakati anaopenda kwa vitisho vyake.

Aurangzeb alisema uchaguzi mpya utatangazwa na serikali yake kwa ushirikiano na makubaliano na washirika wote.

XS
SM
MD
LG