Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 12:14

Wabunge Iran wanamsihi Rais wao kuhusu hakikisho la mkataba wa nyuklia


Mfano wa kiwanda cha nyuklia Iran

Wabunge wa Iran wamemsihi Rais Ebrahim Raisi kupata uhakikisho kutoka kwa Marekani na nchi tatu za ulaya kwamba hazitaondoka kwenye makubaliano ya nyuklia yanayojadiliwa upya mjini Vienna vyombo vya habari vya serikali ya Iran viliripoti Jumapili.

Katika barua kwa Raisi walisema kwamba Marekani na wahusika wa Ulaya kwenye mkataba wa nyuklia; Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, wanapaswa pia kuhakikisha kwamba hazitachochea utaratibu wa haraka ambao vikwazo dhidi ya Iran vitarejeshwa tena mara moja kama inakiuka kanuni za nyuklia.

Tunapaswa kujifunza kutokana na uzoefu uliopita na kuweka mpaka kwa maslahi ya taifa kwa kutoweka ahadi kwa makubaliano yoyote bila kupata dhamana muhimu kwanza wabunge walisema kwenye barua hiyo. Taarifa hiyo ilitiwa saini na wabunge 250, kati ya 290 wa Iran.

Haya yanajiri wakati wapatanishi kutoka Iran na pande zilizosalia katika makubaliano hayo ambayo ni Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Russia na China, wanafanya kazi ya kufufua mkataba wa mwaka 2015 ambao uliipatia Iran nafuu ya vikwazo kwa mabadilishano ya kuzuia program yake ya nyuklia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG