Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 00:46

Obama Apendekeza Wataalam Zaidi wa Kijeshi Iraq


Rais wa Marekani, Barack Obama, amependekeza kupelekwa washauri zaidi 450 wa jeshi nchini Iraq, katika juhudi mpya za kuwapa nguvu wanajeshi wa vikosi vya Iraq katika mapambano dhidi ya Islamic State.

Ikulu ya Marekani, “White House,” imeeleza kwamba wataalamu hao wa Marekani wataongezwa katika wakufunzi 3,100 wa Marekani, ambao tayari wapo nchini Iraq.

Pia imeeleza kwamba waziri mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, aliomba Wamarekani zaidi na Pentagon, pia ilitoa pendekezo kama hilo.

Marekani inapanga kufungua mafunzo mapya katika eneo la al-Taqqadum, kambi ya anga iliyopo jangwani ambayo ilihudumu kama kiungo cha shughuli za kijeshi nchini humo.

XS
SM
MD
LG