Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 10:26

Wavulana watatu washikiliwa Uingereza wakitokea Uturuki


Picha ya Maktaba ya wasichana wa Uingereza wanaodaiwa kujiunga na Islamic State.
Picha ya Maktaba ya wasichana wa Uingereza wanaodaiwa kujiunga na Islamic State.

Wavulana watatu wa Uingereza, wanaodaiwa kutaka kujiunga na kundi la msimamo mkali la Islamic State nchini Syria, wamekamatwa mjini London, Uingereza, baada ya kurudishwa kutoka Uturuki.

Idara ya upelelezi ya Uingereza, Scotland Yard, haikutoa utambulisho wao, lakini ilisema watuhumiwa walishikiliwa Ijumaa, katika mji wa Istanbul.

Ripoti za vyombo vya habari vya Uturuki zinasema wasichana hao watatau wawili wakiwa na miaka 17 na mmoja miaka 19, wanaotokea kaskazini magharibi mwa London.

Walikamatwa wakitokea Barcelona, na kushikiliwa baada ya kuhojiwa na polisi wa uwanja wa ndege.

Kukamatwa kwao kunatokea wiki kadhaa baada ya wasichana wengine watatu wa shule kutoka Uingereza, kupata umaarufu wa kimataifa baada ya kukimbia kutoka London, na kwenda Instanbul.

Siku chache baadaye maafisa wa usalama wa uturuki walieleza kwamba wasichana hao wamevuka mpaka kwenda nchi ya vita Syria na kuna uwezekano wamejiunga na kundi la Islamic State.

XS
SM
MD
LG