Mfanyakazi wa afya Mmarekani, aliyeambukizwa Ebola, yupo njiani kuelekea Marekani, kwa matibabu katika Taaasisi ya taifa ya Afya.
Taasisi hiyo imesema mgonjwa huyo ambaye alijitolea kutibu wagonjwa wa Ebola, nchini Sierra Leone, anatarajia kuwasili Bethesda, jimboni Maryland, Ijumaa.
Mfanyakazi huyo atakuwa katika sehemu maalum ya matibabu katika moja ya vyumba maalum vilivyotengenezwa Marekani, kutibu vimelea vya magonjwa hatari.
Afisa wa tasisi hiyo hakutoa taarifa zozote ikiwemo utambulisho wa mgonjwa.
Mapema, afisa mwanamke wa afya kutoka jeshi la Uingereza, ambaye aliambukizwa Ebola, nchini Sierra Leone, alirudishwa Uingereza pamoja na wafanyakazi wawili ambao waliokuwa karibu nae sana.
Wafanyakazi wengine wawili zaidi waliokutana na mwanajeshi huyo ambaye hakutambulishwa wanapimwa nchini Siera Leone, na wanatarajiwa kuondolewa Ijumaa.