Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:24

IOM yakumbwa na uhaba wa fedha


wafanyakazi wahamaji wakiwa kwenye mstari baada ya kuwasili kwa njia ya meli wakisubiri msaada wa IOM.
wafanyakazi wahamaji wakiwa kwenye mstari baada ya kuwasili kwa njia ya meli wakisubiri msaada wa IOM.
Shirika la kimataifa linaloshughulika na Uhamaji – IOM limeonya kuwa lina upungufu wa fedha na hivi karibuni halitakuwa na fedha za kuhudumia maelfu ya wakimbizi kutoka pembe ya Afrika waliokwama Yemen.

IOM yenye makao yake mjini Geneva inaripoti kuwa tayari imelazimika kupunguza matumizi katika programu mbalimbali kwa watu waliokumbwa na mizozo.

Aidha , IOM inaripoti kwamba hali nchini Yemen kwa wahamaji kutoka Pembe ya Afrika ni tete na hali ya nchi wanakotoka ni mbaya na bado wanaendelea kwenda mashariki ya kati kwa matumaini ya kutafuta ajira.

Wimbi kubwa la wahamaji kutoka Pembe ya Afrika imekuwa marambili zaidi kutoka wakimbili elfu 53 mwaka 2010 hadi laki 107 mwaka jana. Wakimbizi wengi wanaowasili wanatoka Ethiopia wakati waliobaki wanatoka Somalia na Eritrea.

Msemaji wa IOM Jumbe Omar Jumbe anasema shirika lake limelazimika kupunguza matumizi makubwa katika programu zake za misaada kutokana na ukosefu wa fedha na kama hali hiyo haitatatuliwa haraka basi kuna uwezekano mkubwa wa kufunga kituo cha huduma huko Yemen.

Jumbe anasema IOM pia imelazimika kuahirisha programu yake ya kurejea kwa kujitolea kwa sababu ya ukosefu mkubwa wa fedha. Anasema ndege ya mwisho ya watu walikuwa wanarejea kwa kujitolea ilikuwa mwezi septemba ambapo wahamiaji 210 walirejea Ethiopia.
XS
SM
MD
LG