Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 13:39

Uganda yasema ripoti ya UN haina msingi.


Ripoti ya UN kwa ajili ya Drc yasababisha upinzani Uganda na Rwanda.
Ripoti ya UN kwa ajili ya Drc yasababisha upinzani Uganda na Rwanda.
Serikali ya Uganda inasema ripoti ya umoja wa mataifa inayodai kuwa Uganda na Rwanda zinafadhili waasi wa M23 mashariki mwa Congo haina msingi wowote na ni ya hovyo. Uganda sasa inataka umoja wa mataifa utoe ushahidi wa kuonyesha kuwa kweli wanajeshi wake wamo mashariki mwa Congo wakiwasaidia waasi wa M23. .

Ripoti hiyo ya umoja wa mataifa ambayo haijachapishwa rasmi na shirika hili ilichapishwa jumanne na shirika la habari la Reuters. Ripoti hii inasema Uganda imekuwa ikiwasaidia waasi wa M23 ambao wamekuwa wakipigana na serikali ya demokrasia ya Congo.
Waasi hawa waliteka sehemu kubwa za mashariki mwa Congo na wanatarajiwa kuwateuwa machifu watakao viongoza vijiji vya maeneo waliyoyateka.

Madai ya kuwa Uganda inafadhili kundi la M23 hayakupokelewa kwa mikono mikunjufu mjini Kampala. Kanali Felix Kulayigye ni msemaji wa jeshi la Uganda alisema ni jambo la kuhuzunisha kuona ripoti kama hii ikichapishwa na umoja wa mataifa.
Alisema wapo watu wanaofanya kazi na umoja wa mataifa ambao hawataki usalama urejeshwe mashariki mwa Congo na sasa wameanza kusambaza fununu ili wazidi kuwa na ajira.

Kulayigye anasema kati ya nchi zote za Afrika, Uganda inasifika kwa kuwa kwenye mstari wa kwanza wa kuhakikisha kuwa usalama unapatikana kwenye nchi zisizo na usalama. Kila wakati Uganda huwa tayari kutuma wanajeshi wake kupigana kutetea usalama wan chi hizo.
XS
SM
MD
LG