Serikali ya Haiti iliomba rasmi msaada wa usalama kutoka kwa nchi zote kote duniani, zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Uchumi wa Rwanda unatarajiwa kukua kwa asilimia 6.6 mwaka 2024, ikilinganishwa na mwaka huu ambapo umekuwa kwa asilimia 6.2, Waziri wa fedha na Gavana wa Benki kuu wameandika barua kwa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani- IMF.
Kampuni ya kutengeneza chanjo za Covid-19 ya BioNtech inalenga kuanza utengenezaji kwenye kiwanda chake cha chanjo cha mRNA chini Rwanda kufikia 2025, maafisa wake wamesema Jumatatu, ikiwa kampuni ya kwanza ya kigeni kutengeneza chanjo hizo barani Afrika.
Tume ya uchaguzi ya Rwanda imesema Jumanne kwamba uchaguzi wa Rais na bunge utafanyika Julai 15 mwaka ujao, wakati rais Paul Kagame akiwania kwa mhula wa nne.
Waziri Mkuu wa Uingereza alikuwa anahangaika siku ya Jumatatu kutafuta kura za kutosha kwa ajili ya sera yake uhamiaji ya kuwapeleka wanaoomba hifadhi nchini Rwanda baada ya wabunge wa chama chake kusema mpango wa sheria ya dharura hauna nguvu ya kutosha
Migawanyiko imeibuka katika chama cha Conservative juu ya mpango wake wa kisheria kwa Rwanda, kabla ya kuchapishwa kwake.
Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amewataka wabunge wa chama chake cha Conservative siku ya Alhamisi kuunga mkono mpango wake wa kuwapeleka Rwanda waomba hifadhi baada ya mpango huo kukataliwa na kubainisha migawanyiko mikubwa ndani ya chama chake.
Msemaji wa serikali ya Rwanda ametangaza kutokubaliana na uamuzi wa mahakama ya juu nchini Uingereza wa kukataa kuwapeleka wahamiaji haramu nchini Rwanda.
Mahakama ya Juu ya Uingereza Jumatano imetoa maamuzi kwamba mpango wa serikali wa kuwapeleka baadhi ya wahamiaji nchini Rwanda ni kinyume cha sheria.
Takriban watu 15 wamefariki dunia nchini Kenya wakati mafuriko yaliposomba nyumba nyingi na kuharibu mashamba kufuatia mvua kubwa, Shirika la Msalaba Mwekundu lilisema Jumatatu.
Rwanda Alhamisi imetangaza kwamba itawaruhusu waafrika kuingia nchini humo bila ya visa, likiwa taifa la karibuni la katika bara hilo kuchukua hatua inayolenga kuimarisha usafiri wa watu na bidhaa, sawa na ilivyo barani Ulaya kwenye eneo la Schengen.
Wanajeshi wawili wa Uganda wamelazwa hospitalini wakiwa katika hali mahtuti baada ya kupigwa risasi na kundi la waasi masahriki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Pandisha zaidi