Poland ilisema Jumapili kwamba itaitaka Russia kueleza ukiukaji mpya wa anga baada ya kombora la Russia kuingia kwenye anga ya nchi hiyo ya NATO kwa takriban kilomita 2 Jumapili asubuhi kabla ya kurejea Ukraine, kulingana na msemaji wa jeshi la Poland.
Chama kikuu cha upinzani nchini Burundi kilikumbwa na mgawanyiko Jumapili baada ya tawi lake kusema kuwa limemuondoa kiongozi wa chama hicho Agathon Rwasa kwa kushindwa kuunganisha pande mbili zinazolumbana.
Serikali ya Haiti iliomba rasmi msaada wa usalama kutoka kwa nchi zote kote duniani, zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Msemaji wa serikali ya Burundi amesema Jumatatu kwamba watu wenye silaha kutoka kundi la waasi la Red Tabara wameua watu 9 na kujeruhi wengine kwenye mashambulizi ya usiku kucha magharibi mwa mwa nchi karibu na mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Uchumi wa Burundi unatarajiwa kukua kwa asilimia 4.3 mwaka huu kutoka asilimia 2.7 mwaka 2023, ikiwa umesaidiwa na kuboreshwa kwa utendaji katika sekta ya kilimo, Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani -IMF lilisema.
Takriban watu 15 wamefariki dunia nchini Kenya wakati mafuriko yaliposomba nyumba nyingi na kuharibu mashamba kufuatia mvua kubwa, Shirika la Msalaba Mwekundu lilisema Jumatatu.
Wanajeshi wawili wa Uganda wamelazwa hospitalini wakiwa katika hali mahtuti baada ya kupigwa risasi na kundi la waasi masahriki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
India na Tanzania zinatafuta namna ya kuendesha biashara kwa kutumia sarafu zake kutokana na uhaba wa dola duniani.
Mapigano makali yanaendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya kundi lenye silaha linalojiita Wazalendo, ambalo linaungwa mkono na serikali na kundi la M23.
Mahakama nchini Burundi imemnyima dhamana waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Alain-Guillaume Bunyoni, ambaye ameshtakiwa kwa shutuma za kuhujumu usalama wa taifa na kumtusi rais, vyanzo karibu na kesi hiyo vililiambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi.
Wiki hii tunaangazia mkutano kati ya rais wa Russia Vladimir Putin na viongozi wa nchi za Afrika, mapinduzi nchini Niger na Maandamano nchini Israel. Mtayarishaji na msimulizi wa kipindi ni Kennes Bwire
Viongozi wa Afrika wanaanza mkutano wao na rais wa Russia Vladmir Putin, nchini Russia lakini chini ya nusu ya marais wa Afrika wanahudhuria mkutano huo wakisema wanastahili kuakilishwa na mwenyekiti wa umoja wa Afrika hatua ambayo Russia inadai inachochewa na nchi za magharibi.
Pandisha zaidi