Wanamgambo wa Kiislamu wa kundi la al-Shabab Alhamisi walishambulia hoteli maarufu karibu na ikulu ya rais katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, vyanzo vya usalama na mashahidi walisema.
Wagonjwa wamekwama katika hospitali mbalimbali nchini Kenya kufuatia mgomo wa madaktari unaolenga kuwezesha utekelezaji wa mahitaji ya nafasi za lazima za mafunzo ya utabibu kwa zaidi ya madaktari waliohitimu 4,000, ajira na mazingira bora ya kazi.
Serikali ya Haiti iliomba rasmi msaada wa usalama kutoka kwa nchi zote kote duniani, zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Wajumbe zaidi ya 350 wa serikali, taasisi za utafiti na makampuni yanayotengeneza mbegu wanakutana Kenya wiki hii kujadili changamoto za upatikanaji wa mbegu –bora kwa ajili ya wakulima wa Kiafrika.
Rais wa Kenya William Ruto amelitaka bunge la Afrika Mashariki kuendelea kuwa kiungo muhimu katika juhudi za kuimarisha ushirikiano na watu wa Afrika Mashariki na mshikamano wa nchi wanachama ili kuboresha maendeleo ya kijamii na kiuchumi ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki.
Mji mkuu wa Haiti kwa kiasi kikubwa umefungwa, wakaazi wakijitokeza kutafuta mahitaji muhimu huku mamlaka ikiweka hali ya dharura baada ya uvamizi dhidi ya gereza na kusababisha maelfu ya wafungwa kuachiliwa.
Polisi nchini Kenya wamesema Jumanne, kwamba watu wawili wamekufa kwenye ajali kati ya ndege ya chuo cha urubani, na ile ya abiria, kwenye mji mkuu wa Nairobi.
Kenya na Haiti siku ya Ijumaa zimetia saini makubaliano ya pande mbili ya kupeleka polisi kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki, kuongoza kikosi kinachoungwa mkono na UN ili kupambana na magenge ya uhalifu nchini Haiti, amesema William Ruto.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Rais William Ruto wa Kenya wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa raia wa nchi zao, kuondoa vikwazo vya usafiri na kuwezesha kuongezeka kwa biashara kati ya nchi hizo mbili.
Rais wa Kenya William Ruto alikuwa kati ya maelfu ya waombolezaji waliokwenda kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa anashikilia rekodi ya ulimwengu ya mbio ndefu, Kelvin Kiptum siku ya Ijumaa (Februari 23).
Bingwa wa dunia wa mbio za masafa marefu kutoka Kenya Kelvin Kiptum, ambaye ndoto yake ya kuvunja rekodi ya kukimbia kwa muda wa chini ya saa mbili ilikatizwa na ajali ya barabarani mapema mwezi huu, Ijumma amesifiwa na viongozi mbali mbali waliohudhuria mazishi yake magharibi mwa Kenya.
Lugha ya Mama au lugha ya asili ni msingi imara wa kujifunza lugha nyingine. Kwasababu ni lugha ya kwanza ambayo mototo anajifunza nyumbani kabla ya kuanza masomo.
Pandisha zaidi