Jumapili, Februari 14, 2016 Local time: 08:48

  Watangazaji

  Hawa ni watangazaji wako ambao umekuwa ukiwasikia kwenye matangazo ya Sauti ya Amerika.
   

   

  Mwamoyo Hamza, Mkuu wa Idhaa

  Mwamoyo HamazaMwamoyo Hamza ni mtangazaji wa siku nyingi katika Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika. Mzaliwa wa Tanga, Tanzania, Mwamoyo alisomea uandishi
  habari katika Chuo Cha Uandishi wa Habari cha Dar es Salaam, Tanzania na kuanza kazi ya uandishi katika magazeti ya Daily/Sunday News. Baadaye alipata shahada za juu katika uandishi na mawasiliano katika chuo kikuu cha Howard mjini Washington D.C. Alijiunga na VOA mwaka 1994. Mbali na vipindi vya habari Mwamoyo pia anatayarisha makala za kila wiki za "Amerika Leo" na "Jamii na Maendeleo."
   


  Abdushakur Aboud

  Abdushakur Aboud Abdushakur ni mtangazaji wa muda mrefu aliyejiunga na VOA 1992. Yeye ni mzaliwa wa Zanzibar lakini anatokea visiwani Comoro. Alihitimu uandishi wa habari katika chuo kikuu cha Dakar, Senegal, na kupata mafunzo ya utangazaji wa Televisheni huko Ujerumani na Japan. Alifanyakazi na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani, na baadae idhaa ya kiswahili na kingereza ya redio ya Uingereza BBC. Hivi sasa hutayarisha vipindi vya televisheni vya VOA pamoja na vipindi vya "Maswali na Majibu" na Muziki kutoka Afrika."
   


  Esther Githui Ewart

  Ester Githui EwartEsther Githui Ewart ni mtangazaji katika idhaa ya Kiswahili na televisheni ya Sauti ya Amerika . Ni mzaliwa wa Kenya ambaye alisomea uandishi habari katika chuo kikuu cha Nairobi. Kabla ya kujiunga na Chuo hicho alisomea shahada ya elimu katika chuo kikuu cha Kenyatta na kufundisha kwa muda mfupi katika shule mbalimbali za sekondari nchini Kenya . Anafahamika vyema nchini humo ambapo kwa muda wa miaka minane aliandaa vipindi na kusoma taarifa za habari katika shirika la kitaifa la televisheni na radio - K.B.C. Esther alijiunga na Sauti ya Amerika mwaka 2000. Mbali na kazi za kila siku za kuandaa ripoti na taarifa za habari, ni mhariri na mwandalizi wa kipindi kinachopendwa sana “Jarida la Jumapili” ambapo huwaletea mahojiano ya kina ya kijamii, kisia+sa kiuchumi na kitamaduni akiwaalika washiriki mbalimbali kutoka maeneo ya Afrika ya Mashariki; ya kati, Marekani na kwingineko . Amewahoji maafisa wakuu wa serikali ya Marekani juu ya sera ya Marekani kwa Afrika mkiwemo rais George W. Bush mwaka wa 2002 katika ikulu ya White House, Rais mteule Barack Obama wa Marekani, mbunge Maxine Waters wa California miongoni mwa wengine. Kwa starehe zake Esther anapenda kupumzika na familia yake, kusoma na kufuatilia matukio mbalimbali kupitia vituo vya televisheni.
   


  Khadija Riyami

  Khajida Riyami - VOA Swahili BroadcasterKhadija Riyami alijiunga na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika mwaka 1998. Kabla ya hapo alikuwa ni Mhariri wa Michezo katika magazeti ya Daily News/Sunday News nchini Tanzania. Pia aliwahi kuwa mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani - Deutschewell na mwandishi wa kipindi cha michezo cha Fast Track katika Shirika la Utangazaji la Uingereza - BBC. Khadija hivi sasa ni Mhariri na pia anaandaa vipindi vya Dunia ya Wanawake na Matukio ya Afrika. alipata shahada ya uandishi kutoka Chuo cha waandishi wa habari nchini Tanzania na kupata mafunzo ya juu ya uandishi nchini Afrika Kusini, Ujerumani na Uingereza.
   


  Sunday Shomari

  Sunday Shomari Sunday Shomari ni mzaliwa wa Daressalaam Tanzania na alianza kazi ya utangazaji katika kituo cha radio one na ITV mjini Daresalaam akiwa anatangaza Muziki kwenye Televisheni hiyo na vipindi mbalimbali kwenye radio.Baadaye alifanya kozi ya utangazaji Marekani na kujiunga na chuo cha uandishi wa habari Tanzania na pia kuandika makala za burudani katika magazeti ya Nipashe na Alasiri na hivi sasa anaendelea na shahada ya mawasiliano katika chuo kikuu cha Maryland. Alijiunga na Sauti ya Amerika 2008 ambapo mbali na vipindi vya habari anaandaa kipindi cha Burudani kila Jumamosi.