Jumamosi, Februari 06, 2016 Local time: 10:09

  Simu

  Sauti ya Amerika (VOA)inakupatia habari mpya kwenye simu yako ya mkononi au kwa chombo chochote kinachopata mtandao wa internet… bila malipo yoyote!

  Ingia kwenye tovuti m.voanews.com/swahili katika mtandao wa internet kwa kutumia simu yako au PDA na utaweza kupata habari za VOA kwa kutumia simu yako ambayo ina huduma ya internet. Usisahau kualamisha tovuti hii kwenye simu yako.

  MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA

  • Vipi naweza kuipata VOA kwa kutumia simu yangu ya mkononi, PDA au chombo kingine cha mkononi?
  • VOA inatoa huduma gani kwa simu za mkononi au simu maalum ?
  • Je VOA inatoza fedha kwa kupata habari kwa njia ya simu ya mkononi?
  • Nimeingia kwenye tovuti  m.voanews.com/swahili , lakini nimeshindwa kuusoma ujumbe.

   

  Vipi naweza kuipata VOA kwa kutumia simu yangu ya mkononi, PDA au chombo kingine cha mkononi?

  Unaweza kupata habari za VOA bure kutoka kwenye simu yoyote ya mkononi au chombo kingine cha mkononi ilimradi unayo huduma inayokuwezesha kuingia kwenye mtandao wa internet kwa ajili ya simu za mkononi. Kuipata VOA ingia kwenye tovuti m.voanews.com/swahili kwa kutumia simu yako ya mkononi. Mara unapoingia katika ukurasa wa habari za VOAkwa njia ya simu, alamisha ukurasa huo ili mara nyingine unapotaka kuingia katika ukurasa huu itakuwa haraka zaidi ili uweze kupata habari mpya kutoka VOA.

   

  VOA inatoa huduma gani kwa simu za mkononi au simu maalum?

  Katika ukurasa wa m.voanews.com/swahili utakuta habari kuu za siku. Kama unataka habari maalum kwa kuchagua eneo la kijiografia, utakuta kiungo maalum cha kukuunganisha na habari za VOA kuhusu Afrika, Siasa, Afya, Vita na Migogoro, Maswala ya Kijamii, Haki za Binadamu na Sheria.

   

  Je VOA inatoza fedha kwa kupata habari kwa njia ya simu ya mkononi?

  Huduma yaVOA ya habari kwa njia ya simu inatolewa kwa wasomaji wetu bila gharama. Makampuni yanayotoa huduma ya simu za mikononi au PDA kwa kawaida wao hutoza gharama kwa kutumia huduma ya internet. Wasiliana na kampuni inayokupatia huduma ya simu ya mkononi kwa maelezo zaidi kuhusu gharama za matumizi ya internet.

   

  Nimeingia kwenye tovuti m.voanews.com/swahili, lakini nimeshindwa kuusoma ujumbe.

  m.voanews.com/swahili inapatikana katika lugha mbali mbali na inatumia seti maalum za kila lugha. Kama simu yako ya mkononi au PDA haiwezi kuonyesha ujumbe kwa lugha hiyo, unatakiwa kuwasiliana na kampuni inayokupatia huduma hiyo au muuzaji wa PDA ili aweze kufanya marekebisho maalum ili kupata huduma hiyo. Habari zote katika m.voanews.com/swahili zimefanyiwa majaribio kuona kuwa zinafanya kazi kwenye simu za aina tofauti, hata hivyo pengine simu za zamani huenda zisiwe na viwango vya sasa vya tovuti. Kama unapata shida kuona lugha unayoitaka, tafadhali tujulishe ni ipi. Kwa kuongezea, kama unaweza kuona mitandao mingine ya simu za mkononi katika lugha hiyo hiyo, tujulishe tufahamu tovuti ipi ndiyo inaonyesha ujumbe huo kwa usahihi. Tafadhali tujulishe na tuletee maoni au maswali uliyo nayo kuhusu m.voanews.com/swahili kwa kutuletea ujumbe wa barua pepe voaswahili@voanews.com Tafadhali hakikisha unaonyesha ni gani ambako unatumia huduma hii, kampuni ya simu yako mkononi na mtengenezaji wa simu na namba ya muundo wa simu unayoitumia.