Ijumaa, Machi 27, 2015 Local time: 14:55

Habari / Afrika

Watu 39 wauwawa Kenya

 • Wakazi na polisi watizama miili ya wanaotuhumiwa ni washambulizi kutoka kabila la Pokomo, kufuatia mapambano ya kikabila katika kijiji cha Kipao wilaya ya Tana River Delta kusini mashariki ya Kenya. Dec. 21, 2012.
 • Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundi wakimbeba mtu aliyejeruhiwa wakati wa shambulizi katika kijiji chake wilayani Tana River.
 • At least 39 people including men, women, children, and attackers, were killed when farmers from the Pokomo tribe, armed with spears and AK-47 rifles, raided a village of semi-nomadic Orma herders early Friday, according to a police official.
 • Paramedics at the Malindi district hospital attend to a child injured when their community members were attacked at Tana River district in Kenya's coastal Tana Delta region December 21 2012.
 • Children injured during an attack in their village in Tana River district receive treatment inside a ward at the Malindi district hospital December 21, 2012.
 • An injured woman is treated at the district hospital in Malindi Friday, Dec. 21, 2012, following tribal clashes in Kipao village in the Tana River Delta.
 • A villager armed with a spear walks past Kenyan police sent to keep order following tribal clashes in Kipao village in the Tana River Delta region of southeastern Kenya.
 • A villager walks away armed with a spear after viewing the bodies of suspected attackers from the Pokomo tribe, not pictured, following tribal clashes in Kipao village in the Tana River Delta region.

Maafisa wa serikali nchini Kenya wanasema watu wasiopungua 39, wanavijiji 30 na washambuliaji tisa wameuwawa katika mapambano mengine  mapya kati ya makundi mawili hasimu ya kikabila katika mkoa wa kusini mashariki wa Tana River.
 
Ofisa mmoja wa polisi katika eneo anasema kundi la kabila la Pokomo lililokuwa limebeba mishale na bunduki  lilivamia kijiji cha watu wa Orma, alfajiri ya Ijumaa.
 
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya linasema watoto 13 na wanawake sita walikuwa miongoni mwa waliouwawa katika shambulizi kwenye kijiji cha Kipao. Inasema kiasi cha nyumba 45 zilichomwa moto.

Polisi wanasema wanafahamu  mahali washambuliaji wanakotoka na wanawafuatilia.Makundi hayo mawili yamefanya mifululizo ya mashambulizi ya mauaji na mashambulizi mengine kama sehemu ya mgogoro unaoendelea juu ya ardhi na maji.
 
Mwezi wa Agosti na Septemba zaidi ya watu 100 waliuwawa katika mapambano kati ya kabila la Pokomo ambayo ni jamii kubwa ya wakulima na kabila la Orma ambalo linafahamika kwa ufugaji.

Umoja wa Mataifa unasema baadhi ya mauaji huenda yanahusiana na kuongezeka kwa mivutano  kuhusu  uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Zaidi ya watu 1,100 waliuwawa katika ghasia za uchaguzi mkuu uliopita nchini Kenya wa mwaka 2007.
mjadala huu umefungwa
Comment Sorting
Maoni
     
Na: ndombi Kutoka: kenya
31.12.2012 15:18
sura mbaya sana hii kwa taifa kama hili letu kenya ambalo limejulikana sna kwa kuwa amani na utulifu

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Ajali barabarani Tanzania zaongezekai
|| 0:00:00
...  
🔇
X
18.03.2015 16:17
Matukio ya ajali mbaya za barabarani Tanzania hivi karibuni zinasemekana kuwa ishara ya ongezeko la uzembe na kutozingatia sheria za usalama barabarani, kulingana na watalaam.