Jumapili, Aprili 19, 2015 Local time: 04:00

Habari / Afrika

Watu 10 wakamatwa kuhusika na shambulio la Arusha

Shambulio la bomu Arusha, Tanzaniai
X
06.05.2013 20:53
Idadi ya walouliwa kutokana na shambulio la Arusha imefikia watu watatu na watu sita kukamatwa.
Serikali ya Tanzania imetoa taarifa ya awali juu ya shambulizi la bomu katika kanisa katoliki la Mt.Joseph parokia ya Olacity mjini Arusha.

Akitoa kauli hiyo ya serikali  bungeni Dodoma Jumatatu waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Dr.Emmanuel Nchimbi aliwasihi wananchi kuwa watulivu wakati serikali ikiwasaka wale waliofanya shambulio hilo.

Maafisa nchini Tanzania wamewakamata watu 10  ikiwa ni pamoja na raia wanne wa Saudia Arabia .

Shambulizi hilo lilitokea wakati  kanisa hilo jipya lilipofanya misa yake ya uzinduzi iliyohudhuriwa na balozi wa Vatikan nchini Tanzania .

Mashahidi  kutoka kwenye  eneo la tukio wanasema guruneti  lilirushwa kwenye umati wa watu karibu na mlango wa kuingilia kanisani.
Ripoti ya Dina Chahali
Ripoti ya Dina Chahali - 2:29i
|| 0:00:00
...    
🔇
X

Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo ametangaza kukamatwa kwa watu hao siku ya jumatatu.

Hali katika hospitali ya Mount Meru Arusha ilikuwa tete huku madaktari wakifanya kila wawezalo kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa kwa wakati mmoja. Sauti ya Amerika ilizungumza na Daktari Haika Mhando wa Mount Meru na kutaka kujua hali hospitalini hapo.
Hali katika hospitali ya Mount Meru
Hali katika hospitali ya Mount Meru - 2:28i
|| 0:00:00
...    
🔇
X
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Mgomo wa mabasi ya abiria Tanzania VOA MItaanii
|| 0:00:00
...  
🔇
X
10.04.2015 19:18
Mgomo wa madereva ya basi za umaa Tanzania umesababisha usumbufu mkubwa kwa abiria kote nchini.