Jumanne, Februari 09, 2016 Local time: 00:07

  Habari / Afrika

  Mauwaji ya raia na polisi yazusha wasiwasi Tanzania

  Mkutano wa chama cha upinzani cha Chadema kumaliza kampeni za uchaguzi wa 2010 Dar es Salaam
  Mkutano wa chama cha upinzani cha Chadema kumaliza kampeni za uchaguzi wa 2010 Dar es Salaam
  Vyama vya siasa pamoja na taasisi za haki za binadamu nchini Tanzania vimeelezea  wasiwasi wake juu matukio ya mauaji ya raia na askari polisi yanayoripotiwa kutokea katika sehemu mbalimbali nchini katika siku za hivi karibuni.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkurungezi mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dkt Helen Kijo-Simba ametaka serikali na mamlaka husika kuchukulia mauaji hayo hasa ya askari polisi kwa uzito wa kipekee kwani yana athari kubwa katika mustakabali wa amani na utulivu wa nchi.

  Mkurugenzi huyo wa kituo cha sheria na haki za binadamu amesema matukio mengi ya mauaji nchini Tanzania yameongezeka zaidi kwa mwaka huu wa 2012 pengine kutokana pia na kuwepo tatizo katika kufuata  utawala wa sheria kwa waliopewa mamlaka ya kusimamia usalama na amani ya nchi.

  Dakta Bisimba alikuwa akizungumzia matukio mbalimbali ikiwemo mauaji ya askari polisi wawili yaliyofanywa na raia huko Ngara mkoani Kagera , mauaji ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoani Mwanza marehemu Lebaratus barlow na pia mauaji ya askari wa kikosi cha polisi cha kutuliza ghasia huko visiwani Zanzibar na mauaji mengine ya raia wa kawaida katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika mikusanyiko ya kisiasa, iliyosabaisha pia kuuwawa kwa mwandishi wa habari daudi mwangosi.

  Wakati wanaharakati wa haki za binadamu wakitaka hatua hizo dhidi ya mauaji ya raia, chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika moja ya maazimio yake yaliyotokana na kikao cha kamati kuu ya chama hicho kilichoketi hivi karibuni jijini Dar es salaam, kimetaka rais Jakaya Kikwete kuchukau hatua dhidi ya mapendekezo waliyoyatoa ya kutaka aunde mahakama ya kikatiba kushughulikia mauaji ya raia..

  Mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA Freeman Mbowe katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Jumanne, kuzungumzia maazimio ya kamati kuu ya chama hicho pamoja na masuala mengine  amesema wanadhani serikai haifanyi vya kutosha kukabili mauaji ya raia katika maeneo mbalimbali nchini..

  Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo wa taifa wa CHADEMA amewaeleza wanahabari kuwa kamati kuu ya chama hicho imeazimia kutumia njia mbalimbali ikiwemo ya kibunge kupitia hoja binafsi  kuwasilisha bungeni mapendekezo ya marekebisho ya katiba ya mpito kuhakikisha tume huru ya uchaguzi na sheria za uchaguzi zinafanyiwa marekebisho kabla ya katiba mpya ili uchaguzi wa 2015 ufanyike kwa haki..

  CHADEMA imeishutumu serikali na tume ya taifa ya uchaguzi kukwepa wajibu wa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura toka mwaka 2010 hali itakayoathiri haki ya kikatiba ya wananchi kupiga kura na matokeo ya chaguzi za marudio zinazofanyika ambapo wanataka 2013 daftari hilo lifanyiwe marekebisho ili pia litumike katika kura za maoni za katiba mpya.

  You May Like

  Jioni

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
  VOA Express

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo. VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.
  Alfajiri

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

  mjadala huu umefungwa
  Comment Sorting
  Maoni
       
  Na: anania Kutoka: S A
  21.12.2012 01:46
  Hongera sna VOA kwa matangazo yenu na nina hitaji sana mukuwe munanitumia. kama kuna muchango nimi na weza kuchangia.