Jumatatu, Novemba 30, 2015 Local time: 10:57

Makala Maalum / Uchaguzi Kenya 2013

Wakenya wajitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa March

Wapiga kura wajiandikisha kabla ya uchaguzi mkuu
Wapiga kura wajiandikisha kabla ya uchaguzi mkuu
Kenya imekuwa ikifanya mageuzi makubwa ya kisiasa na katiba kufuatia ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. 

Katiba mpya iliandikwa kupendekeza mageuzi kamili ya mfumo wa sheria na kisiasa nchini Kenya na kuidhinishwa na wananchi kwa kura ya maoni hapo Agusti 4 2010.

Tangu wakati huo mageuzi muhimu ya sheria na mfumo wa kisiasa lianza kutekelezwa na utaratibu huo wote utafikishwa kikomo tarehe 4 March wakati wananchi watapiga kura kuchaguwa utawala mpya chini ya mfumo mashuhuri unaojulikana kama 'Ugatuzi'.

M. Gikonyo anaripoti juu ya utaratibu wa uchaguzi
M. Gikonyo anaripoti juu ya utaratibu wa uchaguzii
|| 0:00:00
...    
 
X

Ugatuzi ni mfumo wa kupeleka serikali kwa wananchi na kuondowa kabisa siasa za kikabila zilziosababisha ghasia na mauwaji ya mwaka 2008.

Macho ya dunia nzima yataelekea Kenya kuona ikiwa juhudi hizi za kuleta mageuzi baada ya kusaidiwa na Jumuiya ya Kimataifa itaweza kurudisha uthabiti na ustawi katika moja wapo ya nchi za Afrika iliyokuwa na utulivu na manendeleo imara.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one