Jumapili, Mei 26, 2013 Local time: 05:05

Habari / Afrika

Wakenya 13 wauwawa katika ajali ya mabasi Tanzania

Ernest Mangu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani, TanzaniaErnest Mangu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani, Tanzania
x
Ernest Mangu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani, Tanzania
Ernest Mangu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani, Tanzania
ukubwa wa habari - +
Idadi ya watu walofariki katika ajali ya mabasi mawili karibu na mji wa Tanga Tanzania Ijuma asubuhi imefikia 13. Watu 42 wamejeruhiwa miongoni mwao 14 wako katika hali tabani, watu 29 hawakujeruhiwa.

Walofariki ni miongoni mwa kundi la wanawake wa Kenya kutoka kanisa la Presbyterian Church of East Africa - PCEA kutoka Thika walokuwa wanasafiri kuelekea Dar es Salaam kwa sherehe za kidini Tanzania.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Pwani Tanzania, Ernest Mangu ameiambia sauti ya Amerika kwamba serikali ya Kenya inashirikiana kwa karibu sana na Tanzania na imepeleka ndege maalum kuwasafirisha nyumbani walonusurika.

Mahojiano na Kamada Mangu
Loading
12:00:00 / -:--:--



Bw Mangu anasema, waumini hao walikuwa wanasafiri ndani ya mabasi mawili wakati basi la pili lilipoanguka kando ya barabara na la pili likagongwa na lori lilipokuwa linasimama  kuwasaidia walokuwa ndani ya basi la kwanza.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--