Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:51

Wahamiaji wa kiafrika washambuliwa Afrika Kusini


Waandamanaji nchini Afrika kusini wakishika mabango yanayosomeka "Kila mtu ni mgeni"
Waandamanaji nchini Afrika kusini wakishika mabango yanayosomeka "Kila mtu ni mgeni"

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametowa wito kwa wa Afrika Kusini kusitisha mara moja ghasia dhidi ya wahamiaji kutoka nchi nyingine za Afrika, wakati maelfu ya watu waliandamana Alhamisi mjini Durban kupinga ghasia za hizo.

Mwandishi habari wa kujitegemea huko Johanesburg, Mohamed Guleid ameiambia Sauti ya Amerika kwamba ghasia hizo zilianza wiki mbili zilizopita baada ya Mfalme wa kijadi wa jimbo la Kwazulu Natal, Goodwill Zwelithini kusema wahamiaji kutoka nchi za kiafrika wamejaa huko afrika kusini.

Maandamano ya kupinga chuki dhidi ya wageni Afrika Kusini
Maandamano ya kupinga chuki dhidi ya wageni Afrika Kusini

Maelfu ya wahamiaji wamelazimika kukimbia makazi yao na hivi sasa kuishi katika makambi yanaofadhiliwa na makundi ya kutetea haki za binadam, kufuatia watu watano kuuliwa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Watu wasiopungua 4,000 waliandamana kote Durban, wakipaza sauti zao “kulaani mashambulizi dhidi ya wahamiaji” na kutetea “Umoja wa Afrika” kwenye tukio lililohudhuriwa na wakazi, wanafunzi, na viongozi wa kidini pamoja na wanasiasa.

Mwandishi habari Guleid anasema polisi walilazimika kutawanya wale wanaounga mkono kufukuzwa wahamiaji na wale wanaowaunga mkono kubaki, baada ya maandamano kulaani ghasia hizo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:07:12 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Katika kiunga cha mashariki ya Johannesburg, polisi walifyatua risasi za mpira na gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya karibu watu 200 waliojipanga kuvamia maduka yanayo milikiwa na wageni.

Ghasia za kuwapinga wahamiaji kutoka nchi za Afrika ziliyalenga kwanza maduka yanayomilikiwa na wa-Somalia na wa-Ethiopia. Mashambulizi tangu wakati huo yamesambaa kuelekea dhidi ya wageni wote wa kiafrika na kusababisha wengi kupata khofu na kutojua la kufanya.

Wahamiaji wakiwa kwenye kambi za muda
Wahamiaji wakiwa kwenye kambi za muda

Ghasia hizo zimelazimisha familia nyingi kukimbilia kambi za muda zinazolindwa na walinzi wenye silaha.

Huku kiwango cha watu wasio na ajira na umaskini kikiwa juu nchini Afrika Kusini wahamiaji wanashutumiwa kuchukua ajira za raia wa Afrika Kusini.

XS
SM
MD
LG