Jumamosi, Mei 18, 2013 Local time: 15:38

Habari

Wafuatiliaji wa UN wachunguza vifo Syria

Watu zaidi ya 150 waliuawa katika kijiji cha Tremseh

SYRIA
SYRIA
ukubwa wa habari - +

Timu ya wafuatiliaji wa Umoja Mataifa  nchini Syria imeondoka Damascus Jumamosi  kuelekea katika eneo ambalo watu zaidi ya 150 waliuawa siku ya Alhamis, huku wanaharakati wa upinzani nchini humo wakiripoti mashambulizi mapya kwingineko nchini humo. Timu hiyo iliondoka mji mkuu wa Syria kuelekea kijiji cha Tremseh chenye wakulima wengi wa dhehebu la Sunni katika mkoa wa Hama. Nalo kundi la Syria na kutetea haki za binadamu limeiambia VOA kuwa majeshi ya serikali yanashambulia mji wa Khirbet Ghazaleh kusini mwa nchi Jumamosi. Kundi la upinzani linasema watu 31 wameuawa  katika mashambulizi ya vikosi vya serikali kote nchini humo leo. Ijumaa,mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Kofi Annan alilaumu majeshi ya serikali na makundi ya wanamgambo waliojihami kwa silaha kwa mauaji katika kijiji cha Tremseh. Wanaharakati wa upinzani wanasema mashambulizi ya Alhamis ndiyo ghasia kubwa zaidi kufanywa kwa wakati mmoja  tangu maandamano ya kupinga serikali ya Syria yaanze mwaka jana. Chombo rasmi cha habari huko Syria kililaumu magaidi kwa mauaji hayo.

mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--