Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:04

Waendesha mashtaka wavamia ofisi za benki ya HSBC


Mwanasheria mkuu wa Geneva, Olivier Jornot akiondoka kwenye tawi la Uswiss la benki ya HSBC huko Geneva, Feb. 18, 2015.
Mwanasheria mkuu wa Geneva, Olivier Jornot akiondoka kwenye tawi la Uswiss la benki ya HSBC huko Geneva, Feb. 18, 2015.

Waendesha mashtaka wa Geneva walivamia ofisi za Uswiss za benki ya Uingereza –HSBC na kutangaza rasmi uchunguzi wa kihalifu kutokana na madai ya kusafisha fedha kwa njia zisizo halali.

Uvamizi huo ulifanyika katika ofisi za HSBC Private Bank (Switzerland) kulingana na taarifa iliyotolewa jumatano na mwendesha mashtaka wa Geneva.

Waendesha mashtaka walisema wanachunguza madai ya utaratibu a hali ya juu wa “kusafisha” fedha kwa njia zisizo halali dhidi ya benki hiyo lakini alisisitiza kuwa uchunguzi huo unaweza kupanuliwa na kuhusisha watu binafsi wanaoshukiwa kushiriki katika vitendo hivyo.

Jengo la benki ya HSBC
Jengo la benki ya HSBC

Mapema mwezi huu, mtandao mkubwa wa waandishi wa habari waligundua tawi la Uswiss la benki ya HSBC, benki kubwa kuliko zote ulaya, lilikuwa likisaidia wateja kutoka sehemu mbali mbali duniani kukwepa kodi na kuficha mamillioni ya dola katika benki hiyo.

Wateja hao ni pamoja na wafanya biashara ya madawa ya kulevya, wauza silaha na watu maarufu pamoja na wanasiasa.

XS
SM
MD
LG